ILINDE NAMBA YAKO YA WHATS UP NA WIZI WA KIMTANDAO ULIOIBUKA HIVI KARIBUNI
Habari ndugu,
Kumeibuka wizi mpya wa mtandao, ambapo wadukuzi (Hackers) wanaweza kutumia namba yako ya WhatsApp kufanya uhalifu bila wewe kujua, hasa ukiwa ,Admin wa group.
Unakumbushwa kuweka security code kwenye namba yako uliyojiunga nayo WhatsApp ili isiweze kutumika mahala pengine popote (kujiunga WhatsApp kwenye simu nyingine) bila idhini yako.
Cha kufanya ili kuweka ulinzi kwenye namba yako, fuata hatua hizi;
Fungua WhatsApp yako
1) Nenda kwenye settings
2) Halafu kwenye account
3) Two-step verification
4) Ingiza tarakimu 6 za security code
5) Thibitisha tena hiyo security code
6) Ingiza e-mail ya kutumia pindi utakaposahau security code yako
7) Thibitisha tena hiyo e-mail.
Mpaka hapo utakuwa umeilinda namba yako kutumiwa na wadukuzi(Hackers) wa mtandao bila idhini yako.
SAMBAZA LINK HII KUWASAIDIA NA WENGINE
EmoticonEmoticon